App hizi huenda zina nambari yako ya simu



David CameronImage copyrightGETTY IMAGES
Image captionNambari nyingi za simu zimepakiwa kwenye hazina ya app za simu, ikiwemo ya waziri mkuu wa zamani Uingereza David Cameron

Siku hizi, kutokana na tabia ya watu kutumia programu tumishi kwa wingi kwenye simu zao, ni kawaida kwa nambari za simu za watu wenye kupatikana kwa urahisi mtandaoni.
Uchunguzi unaonesha kwamba nambari za watu kama vile waziri mkuu wa zamani wa Uingereza David Cameron, kiongozi wa chama cha Leba Jeremy Corbyn, wasanii na mamilioni ya watu zinahifadhiwa kwenye hazina data ambazo umma unaweza kuchakura.
App kama vile Truecaller, Sync.me na CM Security, huwaomba wanaozitumia kupakia kwenye app hizo orodha ya anwani ambazo wanazo kwenye simu wanapoanza kuzitumia.
Ni kwa njia hii ambapo programu hizi hufanikiwa kuwa na hazina kubwa na majina ya watu na nambari zao za simu.
Kuna app moja ambayo inadai ina zaidi ya nambari za simu bilioni mbili, na nyingine inadai ina nambari za simu zaidi ya bilioni moja.
Baadhi ya app huahidi anayezitumia uwezo wa kuzuia mtu asipigiwe simu na watu wasumbufu na pia kuwawezesha watu kutambua nambari za simu za wato ambao wamewapigia lakini hawajahifadhi nambari zao kwenye simu zao au hawawafahamu.
Kinachowatia wasiwasi wataalamu wanaofuatilia haki kuhusu data ni jinsi maelezo haya hukusanywa na programu hizi.
Nyingi huhifadhiwa katika programu hizo bila wenye namabari hizo za simu kufahamu au kuombwa idhini.
Si lazima pia wewe mwenyewe uwe unatumia app hizo, kwani maelezo yanachukuliwa kutoka kwa marafiki, jamaa au watu wengine mradi tu wawe wamezihifadhi kwenye simu zao.

App hizi hukusanya data kutoka kwa vifaa vingiImage copyrightREUTERS
Image captionApp hizi hukusanya data kutoka kwa vifaa vingi

Huwa kuna wasiwasi kuhusu data na maelezo yanayohifadhiwa na app hizo. Mwaka 2013, app ya 2013 Truecaller ilidukuliwa, ingawa wamiliki wake walisema hakuna maelezo ya umuhimu mkubwa yaliyoibwa.
Mwandishi wa masuala kuhusu usalama wa vifaa vya teknolojia Graham Cluley, anasema watu wanafaa kuwa makini sana katika vitu wanavyosambaza au kuwasilisha kwa programu tumishi kwenye simu au kompyuta.
"Unapopakia anwani zote zilizo kwenye simu yako kwa app fulani, unaweza usiri wa kila mtu ambaye anwani yake ipo hapo hatarini na pia usiri wako mwenyewe."
App nyingi huwa zimeeleza kwenye sehemu ya sheria na masharti kwamba wanaotumia app hizo sharti wawe na idhini kutoka kwa wenye data kabla ya kuisambaza, lakini si wengi hufuata haya.
Previous
Next Post »